Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kumetokea mapigano mapya katika mji wa bandari wa Hodeida nchini Yemen baada ya muungano wa Saudia arabia kuanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Huthi.
Ni mapigano ya kwanza tangu pande zote hasimu zilipoyaafiki makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya usitishaji mapigano mwezi Desemba, wamesema maafisa wa vikosi vya usalama na mashuhuda. Pande zote mbili za wapiganaji wa Kihouthi ambao walikuwa wanashirikiria mji huo muhimu na vikosi vya Saudia arabia vinavyoungwa mkono na Marekani wameonekana kuimarisha mipaka na kusimika mitambo ya kujihami. Mapigano hayo yanakuja siku chache baada ya serikali ya Yemen inayopingwa na wananchi sambamba na washirka wake Saudia Arabia na na nchi 11 za kiarabu, kuanzisha mashambulizi kwa kile walichodai kuwa wapiganaji wa Kihouthi wamevunja makubaliano ya usitishaji mapigano na kukataa kuondoa vikosi vyake kutoka mji huo,ambapo wapiganaji hao wanaoungwa mkono na wananchi wamesisitiza kuwa hawawezi kurudi nyuma na kwamba wataendelea kutetea haki na ardhi za wayemen
Mji wa Hudeida ni mji muhimu sana ambapo Marekani na washirika wake wamefanya kila juhudi za kijeshi kuudhibiti lakini hawakufanikiwam hivyo wanataka kuuchukua mji huo kwa kisingizio cha mazungumzo ya kisiasa.
Mwisho wa habari / 291